(ABNA24.com) Tayari serikali ya Misri imechukua hatua ya awali ambapo imewaita na kuwaonya wanasiasa, wanadiplomasia na shakhsia wa nchi hiyo wanaoukosoa mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne na kuwaonya kuhusiana na matokeo mabaya ya kuupinga mpango huo.
Taarifa kutoka Misri zinasema kuwa, vyombo vya kijasusi vya nchi hiyo vinafuatilia kwa karibu mijadala na makala mbalimbali katika mitandao ya kijamii na kuorodhesha majina ya wanadiplomasia na shakhsia wa nchi hiyo wanaoukosoa mpango huo, hususan wanaokosoa msimamo wa serikali ya Rais Abdul-Fattah al-Sisi kuhusiana na mpango wa Muamala wa Karne.
Ikumbukwe kuwa, Jumanne ya tarehe 28 Januari, Rais wa Marekani, Donald Trump alizindua mpango wa Muamala wa Karne akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.
...........
340